LIVERPOOL ULIMI NJE KWA CARLISLE UNITED, YAPENYA KWA MATUTA …Southampton yaangusha karamu kwa MK Dons, pata matokeo ya mechi zote za Capital One
Kocha wa Liverpool aliye kikaangoni Brenden Rodgers alilazimika kusubiri hadi hatua za matuta ili kusonga mbele kwenye michuano ya Capital One dhidi ya timu dhaifu ya Carlisle United.
Liverpool walikuwa wa kwanza kufunga kupitia kwa Danny Ings, lakini Carlisle United wakachomoa dakika 11 baadae kwa bao la Derek Asamoah.
Matokeo yakabaki hivyo hata pale ziliopoongezwa dakika 30 za 'extra time' na ikabidi mshindi apatikane kwa mikwaju ya penalti ambapo Liverpool ikashinda kwa 3-2.
Nayo Southampton wamewaangushia kipigo kizito wababe wa msimu uliopita wa Manchester United – MK Dons kwa kuwachapa bao 6-0.
Matokeo ya mechi zote za Capital One zilizochezwa Jumatano ni kama ifuatavyo:
Crystal Palace 4 - 1 Charlton Athletic
Milton Keynes Dons 0 - 6 Southampton
Newcastle United 0 - 1 Sheffield Wednesday
Norwich City 3 - 0 West Bromwich Albion
Tottenham Hotspur 1 - 2 Arsenal
Walsall 1 - 4 Chelsea
Liverpool 4 - 3 Carlisle United
Manchester United 3 - 0 Ipswich Town
Comments
Post a Comment