KINDA WA MANCHESTER UNITED ANDREAS PERREIRA AMSHUKURU JUAN MATA KWA KUMWACHIA FREE-KICK ILIYOZAA GOLI
MCHEZAJI chipukizi wa Manchester United, Andreas Pereira amemshukuru Juan Mata kwa kumwachia apige free-kick aliyoitendea haki na kufunga goli dhidi ya Ipswich Town kwenye mtanange wa Kombe la Ligi England (Capital One) Jumatano usiku.
Mtanange huo ulimazika kwa Manchester United kuizabua Ipswich mabao 3-0 na kusonga mbele katika mzunguko wa nne wa michuano hiyo.
Perreira, 19, aliyetinga klabuni hapo miaka mitatu iliyopita alifumania nyavu katika dakika ya 60 akiungana na Wayne Rooney aliyefunga katika dakika ya 23 na Anthony Martial katika dakika ya 90.
Nyota huyo raia wa Brazil alikaririwa akisema goli hilo limeifanya ndoto yake kuwa ya kweli.
Mechi hiyo iliyochezwa katika dimba la Stretford End iliamua hatima ya miamba hiyo ambapo sasa Man Utd itakutana na Middlesbrough Oktoba 26 mwaka huu.
Comments
Post a Comment