Hamis Kiiza 'Diego' ameendelea kufunga kwenye ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara (VPL) baada ya leo kuifungia Simba magoli magoli yote matatu (hat-trick) kwenye ushindi wa goli 3-1 walioupata vijana wa Msimbazi kwenye uwanja wa Taifa wakati wakiwakabili Kagera Sugar kwenye mchezo wa raundi ya tatu ya ligi hiyo.
Goli la kwanza la Simba lilifungwa dakika ya 30 kipindi cha kwanza na Kiiza baada ya Awadh Juma kupiga pasi iliyomkuta Kiiza ambaye moja kwa moja aliukwamisha mpira wavuni.
Goli hilo lilidumu kwa muda wote wa kipindi cha kwanza kwani hadi timu hizo zinakwenda mapumziko Simba walikuwa mbele kwa goli 1-0.
Kipindi cha pili kilianza kwa Simba kufunga goli la pili mfungaji akiwa ni Hamisi Kiiza aliyefunga goli hilo dakika ya 46 kipindi cha pili.
Dakika ya 50 kipindi cha pili, Keneth Masumbuko aliifungia Kagera Sugar goli la pili baada ya mabeki wa Simba Hassan Isihaka na Justice Majabvi kutegeana kumkaba Masumbuko ambaye alifunga goli hilo kirahisi.
Wakati muda ukiwa unaelekea kumalizika, Hamisi Kiiza alifunga goli la tatu katika dakika ya 90 na kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat-trick msimu huu.
Kwenye mchezo wa leo Simba walitengeneza nafasi nyingi za kufunga lakini Ibrahim Ajib alipoteza nafasi nyingi za kufunga ambazo zingeweza kuwapa Simba magoli mengi mengi zaidi.
Wachezaji wa Simba walioanza: Peter Manyika, Hassan Isihaka, Mohamed Hussen, Emery Nimuboma, Simon Serunkuma, Justice Mjabvi, Awadhi Juma, Said Hamisi Juma, Peter Mwalyanzi, Ibrahim Ajib na Hamis Kizza
Wachezaji wa akiba: Vicent Angban, Hassan Ramadhani, Said Issa, Mwinyi Kazimoto, Pape Abdoulaye Ndaw, Boniface Maganga na Joseph Kimwaga.
Kikosi cha Kagera Sugar kilichoanza: Agathon Anton, Salum Kanoni, Said Hassan, Ibrahim Job, Deogratius Julius, George Kavilla, Iddy Kurachi, Laulence Mugia, Mbaraka Yussuph, Daudi Jumanne, Paul Ngaliyoma 8
Wachezaji wa akiba: Abuu Hashim, Aboubakari Mtilo, Erick Kihaluzi, Babuu Ally, Keneth Masumbuko, Lambele Jarome, Rashid Loshuwa.
Comments
Post a Comment