JUVENTUS YAICHINJA MAN CITY EDIHAD



JUVENTUS YAICHINJA MAN CITY EDIHAD

Alvaro MorataMatajiri wa jiji la Manchester, Manchester City wameshindwa kutamba kwenye uwanja wao wa nyumbani Etihad baada ya kukubali kulazwa kwa kipigo cha goli 2-1 dhidi ya Juventus ya Italia kwenye mchezo wa UEFA Champions League ikiwa ni mchezo wa kundi D.

Vijana hao wa Sheikh Mansour waliuhusu magoli yote mawili kwenye dakika 20 za mwisho mbele ya Juventus ambayo hijashinda hata mchezo mmoja wa ligi ya Italia (Seia A) tangu ilipoanza.

 Alvaro Morata na Mario Mandzukic ndio waliihakikishia Juventus ushindi wa ugenini wakati Giorgio Chiellini alijifunga dakika ya 57 kuipa City goli pekee kwenye mchezo huo.



Comments