JOSE MOURINHO AWATAKA WACHEZAJI WAKE WAWE MAKINI NA MANENO YA KUAMBIWA


JOSE MOURINHO AWATAKA WACHEZAJI WAKE WAWE MAKINI NA MANENO YA KUAMBIWA
Blues boss Jose            Mourinho looks on during training at the club's Cobham base on            Monday afternoon 
KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Chelsea, Jose Mourinho amesema kuwa hana ugomvi na kocha wala mchezaji yeyote yule.

Alisema watu ambao wamekuwa wanaeneza habari kuwa yeye ana ugomvi na baadhi ya wachezaji wake, si kweli na wamekosa mambo ya kufanya.

"Mimi nipo huru, sina ugomvi wala chokochoko na mtu yeyote, zaidi ya kutumia muda wangu kufanya kazi yangu," alisema.

Hata hivyo, kocha huyo amewaonya wachezaji wake kuwa makini na watu wenye kupenyeza maneno yasiyofaa, kwavile yanaweza kusababisha matatizo dhidi yao na yeye.


Comments