Kipa wa Porto ya Ureno Iker Casillas atakuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi Champions League Jumanne usiku pale atakaposimama langoni dhidi ya Chelsea.
Huo utakuwa mchezo wake wa 152 ambao umtamfanya amwache nyuma nyota wa zamani wa Barcelona Xavi aliyecheza mechi 151.
Casillas, aliyecheza kwa miaka 16 ya mafanikio makubwa Real Madrid, alicheza mchezo wake wa 151 wakati Porto ilipotoka sare ya 2-2 na Dynamo Kiev.
Iker Casillas anatarajia kuwa mchezaji aliyecheza mechi nyingi zaidi Champions League
Kipa wa Porto Iker Casillas anatarajiwa kuwa kikwazo kwa Chelsea ya Mourinho Jumanne usiku kwennye uwanja wa Estadio do Dragao
Casillas alicheza mchezo wake wa 150 katika Champions League akiwa na Real Madrid katika nusu fainali dhidi ya Juventus
Comments
Post a Comment