Bondia Floyd Mayweather alfajiri ya kuamkia leo alitazama mbingu kabla ya kutangazwa mshindi wa pambano lake analodai ni la mwisho katika career yake ya ngumi dhidi ya Andre Berto katika ukumbi wa MGM grand arena.
Akitoa ishara za kuaga kama alivyodai miezi kadhaa iliyopita, Floyd maarufu kama T.B.E 'The Best Ever' alitangazwa mshindi na majaji wote wanne, huku wawili wakimpa points 118/110 wengine, 117/111 na 120/108.
Ushindi huo wa Floyd Mayweather unamfanya afikishe mapambano 49 bila kupigwa na kuweka historia ya aina yake huku ikizuka mijadala ya nani bondia bora wa muda wote katika ulimwengu wa ngumi.
Katika pambano hilo, kama kawaida yake Floyd hakurusha makonde mengi kwa Berto na baada ya kurusha ngumi chache za ushindi akaanza kumkwepa mpinzani wake hadi pambano lilipofikia mwisho.
Maswali yaliyopo hivi sasa ni je? Floyd kastaafu kweli? Hatorudi tena ulingoni? Tutasubiri kuona hilo kwa bondia ambaye ndiye mwenye pesa nyingi kuliko wanamichezo wote kwa ujumla wao.
Comments
Post a Comment