KOCHA wa zamani wa Manchester United, Sir Alex Ferguson amesisitiza kuwa alikuwa sahihi kumkabidhi mikoba David Moyes ambaye alitimuliwa ndani ya msimu huo huo alioingia.
Ferguson aliyasema hayo wakati akizundua kitabu chake 'Leading' katika ukumbi wa Royal Festival jijini London.
Mwalimu huyo mahiri katika medani ya soka alistaafu mwaka 2013 na kumkabidhi Mskochi Moyes na baadaye Louis van Gaal ambapo hali klabu hapo imeendelea kuwa mbaya.
Hivi karibuni alikaririwa akisema tangu amestaafu wamemvurugia kikosi chake huku akiweka bayana kuwa hajawahi kuingilia maamuzi ya makocha hao.
Comments
Post a Comment