FELLAINI ATAKA VAN GAAL AMCHEZESHE NAFASI YA KIUNGO ...asema ushambuliaji si nafasi yake



FELLAINI ATAKA VAN GAAL AMCHEZESHE NAFASI YA KIUNGO ...asema ushambuliaji si nafasi yake
Marouane Fellaini bado anasotea kupata utawala wa uhakika ndani ya Manchester United licha ya kujiunga na klabu hiyo miaka miwili iliyopita akitokea Everton.

Nyota huyo wa kimataifa wa Ubelgiji alishindwa kupata goli hata moja Manchester United chini ya David Moyes kabla hajaibuka msimu uliopita na kufunga magoli sita katika mechi 27.

Lakini bado Fellaini ameshindwa kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza na amekuwa akichezwa na kocha Loius van Gaal katika nafasi tofauti ikiwemo ya ushambuliaji ambayo Fellaini amesisitiza kuwa sio nafasi yake.

Fellaini mwenye umri wa miaka 27 amenukuliwa akisema: "Wakati kocha anaponitaka nicheze katika nafasi yoyote ile, ninacheza. Lakini nafasi yangu niipendayo ni kiungo,"

Belgian midfielder Marouane                  Fellaini (left) is still struggling to find his true                  identity at Manchester United
 Marouane Fellaini (kushoto) bado hajaona mwanga Manchester United
Fellaini attempts to dribble                  past two Ipswich Town players during United's 3-0                  victory on Wednesday night
Fellaini amesisitiza kuwa nafasi anayoimudu ni ya kiungo






Comments