Naye katibu mkuu wa mabingwa wa michuano hiyo timu Faru Jeuri Bw. Gombela Athuman amesema, siri ya mafanikio yao hadi wanachukua ubingwa wa mashindano ya Ndondo Cup ni ushirikiano waliokuwa nao kwenye timu pamoja na kupanga mambo yao kwa pamoja.
"Ushirikiano ndio siri ya mafanikio yetu, tusingeweza kupata haya mafanikio kama tungekua hatushirikiani. Hakuna kitu kingine zaidi ya ushirikiano na kukaa kupanga mabo kwa pamoja", amesema Athuman.
"Zawadi hii tuliyoipata ya shilingi milioni tano tutatoa kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya kufanya sherehe ndogo ya kupongezana kwa wale wote tuliokuwa tunashirikiana sherehe ambayo inaweza ikafanyika siku ya Jumamosi na kiasi kitakachobaki tutakihifadhi benki kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao".
Comments
Post a Comment