Farid Mussa, Winga wa Azam FC aliyefunga goli la ushindi wakati timu yake ilipocheza mchezo wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara dhidi ya Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi
Baada ya kufunga la goli la pili lililoipa Azam ushindi wa kwanza baada ya kusota kwa sare kwa misimu miwili mfululizo mbele ya Tanzania Prisons, kijana Farid Mussa ameseama amefurahi sana kwa kuifungia timu yake goli muhimu lililoipa pointi zote tatu dhidi ya timu ambayo imekuwa ikiwasumbua kwa muda mrefu kwenye ligi kuu Tanzania bara.
"Namshukuru Mungu nimefunga goli langu la kwanza kwenye mechi ya kwanza ya ligi msimu huu goli ambalo ni muhimu lililotupa ushindi dhidi ya timu ambayo mara zote imekuwa ikitusumbua sana kwenye ligi", ameseam Farid.
"Prisons walivyosawazisha goli wakaanza kucheza na matokeo wakitaka mchezo umalizike kwa sare ya goli 1-1, maana wote walirudi nyuma kuanza kuzuia. Kwasababu sisi tulikuwa tunataka ushishindi, ikabidi tuwashambulie muda wote na hatimaye tukafanikiwa kupata ushindi".
"Sasahivi tunataka ushindi kila mechi, tumejiandaa vizuri na mwalimu anaendelea kutupa maelekezo kulingana na mechi tunayokutana nayo mbele yetu. Itapendeza sana kama tutakuwa mabingwa msimu huu kutokana na maandalizi tuliyofanya kabla ya kuanzan kwa ligi".
Comments
Post a Comment