Chama kinachosimamia soka nchini Uingereza kimeanzisha uchunguzi juu ya manager wa Chelsea na akipatikana na makosa anaweza kufungiwa mechi 5.
Tatizo ni lile ambalo lilitokea kwenye mechi ya ufunguzi wa EPL ambapo inasemekana baada ya kupishana na doctor wa timu, Mourinho alimtolea maneno ya matusi Dr Eva Carneiro.
Gazeti la The Independent limetoa hii ripoti na kutokana na sheria za FA ni kwamba mchezaji au kocha akikutwa na kosa la kutumia lugha ya matusi au ishara ya matusi, adhabu ya ndogo ni kufungiwa mechi 5.
Kama manager Jose akikutwa na hii idhabu, Chelsea itaingia uwanjani bila kocha wao mkuu ndani ya mechi 5 au adhabu nyingine yoyote itakayotolewa.
Comments
Post a Comment