Hali si shwari Chelsea, kipigo cha ba0 3-1 kutoka kwa Everton kimechafua hali ya hewa huku ikionekana wazi jitihada za mabingwa hao kutetea taji lao, zinakumbana na vigingi vingi.
Tajiri asiye na subira Roman Abramovich, Ijumaa alikutana na kocha Jose Mourinho katika kile kilichobashiriwa kuwa ni gumzo kuhusu mwenendo wa timu, lakini matokeo haya ya Jumamosi yanatajwa kuwa yamezidi kumtia 'kizunguzungu' kibopa huyo wa Kirusi.
Steven Naismith aliyetokea benchi, akawa mwiba kwa Chelsea pale aliposimika mabao yote matatu ya Everton kwenye mchezo huo mkali wa Premier League.
Mashabiki wa Everton waliofurika kwenye uwanja wao wa Goodison Park, wakamdhihaki Mourinho kwa kumwimbia: "Unafukuzwa kazi kesho asubuhi", hiyo ikiwa ni baada ya Smith kufunga bao la tatu kunako dakika ya 83.
Smith aliyeingia dakika ya 9 kuchukua nafasi ya Muhamed Besic nafasi ya aliyeumia, alifunga goli lake la kwanza dakika ya 17 kabla ya kutupia la pili dakika tano baadae huku kiungo Nemanja Matic akifunga bao pekee la Chelsea dakika ya 36.
Sentahafu kinda John Stones aliyewaniwa na Mourinho kwa udi na uvumba bila mafanikio, alikuwa kikwazo kikubwa kwa Chelsea.
Sentahafu wa Everton John Stones (katikati) akiruka juu kuzuia mpira kwa kichwa
Hiki kinakuwa kipigo cha tatu kwa Chelsea tangu msimu huu uanze na kufanya ijikusanyie pointi 4 katika jumla ya mechi tano na kuporomoka hadi nafasi ya 16 kwenye msimamo wa Ligi Kuu.
Everton (4-3-3): Howard 7, Coleman 7 (Funes), Jagielka 8.5 (c), Stones 8, Galloway 7, Barry 8, McCarthy 7, Besic 5 (Naismith 9), Barkley 7.5, Kone 7 (Lennon 6), Lukaku 7.5
Chelsea (4-2-3-1): Begovic 7; Ivanovic 4, Zouma 5, Terry 5 (c), Azpilicueta 5; Mikel 4 (Kenedy 5), Matic 8; Pedro 5 (Falcao 5), Fabregas 4 (Willian 5), Hazard 5.5; Costa 4
Naismith akitupia bao la pili kutoka nje ya 18
Hili goli la tatu la Naismith
Nemanja Matic akishangilia bao pekee la Chelsea
Comments
Post a Comment