Karibia kila mpenda soka hajafurahishwa na kitendo cha bwana Costa akiwa mchezoni jinsi anavyosabisha hadi wenzake wanapata kadi nyekundu. Japokua wakati mwingine linaweza kuwa kosa la kweli, lakini linaweza kuwa limechangiwa kwa kiasi kikubwa cha mchezaji huyu.
Kurt Zouma mchezaji mwenzake wa Chelsea alisema kwenye mahojiano na kituo cha television kuhusu hii ishu, "Zuma alisema kwamba hashangai kwasababu anamjua Diego, kila mtu anamjua Diego ni mchezaji ambae anaependa ku-cheat na kumuweka mpinzani wake nje ya mchezo"
Maneno hayo yalisambaa sana na kuwashangaza watu kwamba hata mchezaji mwenzake anamjua Costa ni mtu ambae anapenda sana ku-cheat akiwa uwanjani.
Lakini baadae Kurt Zouma alitumia page yake ya twitter na kusema kwamba alikosea kusema hivyo kwasababu English sio lugha yake ya kwanza. Hakumaanisha alichokisema. Hizi ni tweet zenyewe.
Comments
Post a Comment