Kikosi cha Chelsea kimeibukia kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya baada ya mwanzo mbovu wa ligi ya EPL, kikosi hicho cha Mourinho kimepata ushindi wa goli 4-0 dhidi ya Maccabi Tel Aviv usiku wa Jumatano kwenye uwanja wao wa nyumbani wa Stamford Bridge.
Kiungo wa Chelsea Eden Hazard alikosa penati dakika za mwanzo za kipindi cha kwanza lakini Willian aliifungia Chelsea goli la kwanza kwa mpira wa adhabu ndogo kabla ya Oscar kutupia goli la pili kwa mkwaju wa penati.
Diego Coata akaifungia Chelsea goli la tatu huku Cesc Fabregas akimalizia goli la nne kuipa Chelsea ushindi mnono kuelekea mchezo wao wa EPL mwishoni mwa wiki dhidi ya Arsenal utakaopigwa siku ya Jumamosi.
Comments
Post a Comment