CHELSEA HALI TETE, YABANWA MBAVU TENA


CHELSEA HALI TETE, YABANWA MBAVU TENA

Everton vs ChelseaChelsea wametokota leo mbele ya Everton baada ya kutandikwa kama wamesimama mabao 3-1, mchezo uliopigwa katika dimba Goodison Park, maskani kwa Everton.

Shujaa wa Everton katika mchezo wa leo alikuwa ni 'super sub' Steven Naismith ambaye amefunga magoli yote matatu 'hat-trick'.

Naismith aliingia kuchukua nafasi ya Muhamed Besic baada ya kupata maumivu ya misuli ya paja 'hamstring' na ndipo alipoanza kuandika karamu yake ya mabao kwa klabu yake.

Naismith alifunga magoli yake katika dakika ya 17′, 22′, 82′. Chelsea walipata bao lao kupitia kwa kiungo wake mkabaji Mserbia Nemanja Matic mnamo dakika ya 36'.

Vikosi vilikuwa hivi: Everton (4-3-3): Howard, Coleman, (Funes), Jagielka, (c), Stones,  Galloway, Barry, McCarthy, Besic, (Naismith), Barkley, Kone, (Lennon), Lukaku.

Sub ambazo hazikutumika: Robles, Mirallas, Deulofeu, Osman.

Magoli: Naismith 17′, 22′, 82′.

Chelsea: (4-2-3-1): Begovic, Ivanovic, Zouma, Terry (c), Azpilicueta, Mikel, (Kenedy), Matic, Pedro, (Falcao), Fabregas 4 (Willian), Hazard, Costa.

Sub ambazo hazikutumika: Blackman, Remy, Cahill, Loftus-Cheek.

Mfungaji wa goli: Matic 36′.

Refarii: Andre Marriner

Everton vs Chelsea 1

Picha zaidi ingia hapa



Comments