Kocha wa Liverpool Brendan Rodgers yuko katika wakati mgumu klabuni hapo mara baada ya kushambuliwa na wakongwe wa klabu hiyo kutokana na matokeo mabaya yanayoikabili timu hiyo hivi sasa.
Mara baada ya kukubali kichapo cha mabao 3-1 toka kwa mahasimu wao Manchester United katika dimba la Old Trafford, wachezaji wa zamani wa timu hiyo Jamie Caragher na Graemu Souness wamemshambulia kocha huyo na kukosoa mbinu zake.
Carragher ambaye ni mchambuzi wa soka hivi sasa, amesema klabu inakosa wachezaji wa pembeni lakini Rodgers ameendelea kuutumia mfumo wa 4-3-3 wakati Ibe pekee ndiye mchezaji wa pembeni.
Carragher anasema kwa yeye Coutinho bado sio mchezaji wa pembeni na kwamba kocha wao anahitaji kutumia mfumo unaoendana na aina ya wachezaji alionao kikosini.
Hali si shwari kwa Rodgers msimu huu mara baada ya kutumia pesa za kutosha katika usajili, lakini timu yake haipati matokeo stahiki mara baada ya kupokea vipigo vya goli tatu toka kwa West Ham na sasa Manchester United.
Comments
Post a Comment