Brendan Rodgers anapigania kibarua chake kufa na kupona baada ya wamiliki wa Liverpool FSG kudaiwa kuanzisha mawindo ya kumnasa kocha wa zamani wa Real Madrid Carlo Ancelotti.
Ancelotti, ambaye alishinda taji la Mabingwa Ulaya akiwa na AC Milan na Real Madrid, amefuatwa ili kumbadili Rodgers ambaye amekuwa na mwanzo mbaya msimu huu.
Inaaminika Rodgers bado anasapoti kutoka kwa baadhi ya watu wenye maamuzi Liverpool, lakini sasa kibarua chake kipo kitanzini baada Ancelotti kutupiwa ndoano ili awe mrithi wake.
Liverpool inadaiwa kusaka huduma ya kocha wa zamani wa Real Madrid Carlo Ancelotti baada ya Brendan Rodgers kuwa na mwanzo mbaya wa msimu mpya
Liverpool inajiandaa na maisha bila Rodgers
Comments
Post a Comment