Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Arsenal Robin van Persie amefichua kuwa hana raha na maisha ya Fenerbahce.
Mkali huyo wa kimataifa wa Holand mwenye umri wa miaka 32 hakuanza kwenye mchezo wa ushindi wa 2-1 dhidi ya Bursaspor na ingawa baadae aliingia na kufunga bao la ushindi, lakini aliweka wazi kuwa hakufurahi kuanzia benchi.
Kabla ya mchezo huo, Van Persie alicheza mechi tatu bila kufunga goli ikiwemo mechi ya kipigo cha 3-1 kutoka kwa Molde.
"Kusema ukweli sina furaha kipindi hiki," Van Persie alikiambia kituo cha Lig TV baada ya mechi kumalizika.
"Sikuwa na furaha kuanzia benchi. Niko fiti na nipo kamili kabisa kwa kucheza dakika 90.
"Jibu sahihi ni hiki nilichokifanya, kuisaidia timu kushinda."
Robin van Persie akipongezwa na wenzake baada ya kufunga dhidi ya Bursaspor
Comments
Post a Comment