Lionel Messi amefunga mara mbili na kukosa penalti moja wakati Barcelona ikiifumua Levante 4-1 katika mchezo wa upande mmoja wa La Liga.
Kwa ushindi huo Barcelona inazidi kujikita kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa na pointi 12 baada ya kushinda mechi zake zote nne.
Bao la kwanza la Barcelona lilifungwa na beki wake Marc Bartra katika dakika ya 50, Neymar akapiga la pili dakika 6 baadae kabla ya Messi hajafunga kwa penalti dakika ya 61 huku Levante wakifunga bao la pekee dakika ya 66 kupitia kwa Victor Casadesus.
Messi angeweza kufunga tena kwa penalti dakika ya 76 lakini shuti lake likapaa juu.
Dakika ya 90 uchu wa Messi ukazaa matunda pale alipoifungia Barcelona bao la nne.
Barcelona: Ter Stegen; Alves, Mascherano, Bartra, Adriano; Rakitic, Busquets, Sandro, Munir, Messi, Neymar.
Levante: Ruben, Ivan Lopez, Tono, Camarasa, Verza, Lerma, Juanfran, Roger, Trujillo, Ghilas, Feddal
Lionel Messi (kushoto) na Neymar wamecheza bila pacha wao Luis Suarez - lakini bado wakashinda
Marc Bartra akishangilia bao la kwanza
Messi (kulia) akiifungia Barcelona bao tatu kwa penalti
Neymar akimpa heshima beki wa Barcelona, Rafinha ambaye ni majeruhi na atakuwa nje ya dimba kwa msimu mzima
Comments
Post a Comment