Barca na tatizo la kodi: Baada ya Neymar, Messi, huyu mchezaji mwingine na kesi ya kodi


Barca na tatizo la kodi: Baada ya Neymar, Messi, huyu mchezaji mwingine na kesi ya kodi

Klabu bingwa ya soka nchini Hispania na mabingwa wa ulaya, klabu ya FC Barcelona imeendelea kukumbwa na mzuka wa kesi wa ukwepaji kodi kwa mara nyingine tena.

  Siku mbili baada ya taarifa kusambaa kwenye mitandao juu ya kesi ya ukwepaji kodi inayomhusu Neymar Jr nchini Brazil, leo hii kiungo wa kiargentina anayekipiga katika timu hiyo Javier Mascherano amefunguliwa mashtaka mawili ya ukwepaji kodi na muendesha mashtaka wa mahakama ya Hispania, baada ya kugundulika kukwepa kodi inayofikia kiasi cha €1.5 million.

Inasemekana Mascherano alijaribu kuficha mapato yake kutokana na haki za matumizi ya taswira yake aliyoyapata kutoka kwenye makampuni kutoka USA na Ureno.

  
Makosa hayo aliyafanya katika miwili tofauti, anatuhumiwa kukwepa kodi ya kiasi cha  €587,822.01 mwaka 2011 na  €968,907.76 mwaka 2012.

Kesi hiyo inaweza kuendelea mbele, lakini kwa mujibu wa ESPN washauri wa masuala ya sheria wa Mascherano wanamshauri mchezaji huyo kukiri kosa ili apunguziwe adhabu.

Inasemekana Mascherano ameshalipa sehemu ya kodi kwa kutoa kiasi cha €200,000 mwezi huu  na riba juu. Kiungo amegoma kuzungumzia tuhuma hizo hadharani.

Kampuni aliyotumia nchini Ureno ipo Madeira, ambapo wachezaji wanaocheza Spain  wanaona sehemu nzuri ya kufichia madhambi yao. Serikali ya Spain imekuwa kwenye msako mkali wa uchunguzo kwa wachezaji wanaokwepa kodi. 

Wachezaji wengine wa Barcelona ambao hivi karibuni wameingia kwenye mkono wa sheria ni Lionel Messi na Neymar ambaye juzi iliripotiwa mali zake zimeshikwa kutokana na kukwepa kodi.



Comments