BALOTELLI AANZA KUTAMBA NYUMBANI


BALOTELLI AANZA KUTAMBA NYUMBANI

BalotelliMario Balotelli amefunga goli lake la kwanza tangu arejee tena AC Milan kwa mkopo akipiga mpira wa adhabu ndogo nje ya boksi wakati timu yake ilipoibuka na ushindi wa goli 3-2 dhidi ya Udinese kwenye ligi ya Serie A Jumanne usiku.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 25 alipelekwa AC Milan kwa mkopo baada ya kuwa na wakati mgumu kwenye klabu hiyo ya Merseyside akiwa amefunga magoli manne pekee tangu ajiunge na Liverpool. Balotelli alifunga goli la kwanza akiwa umbali wa mita 30 kutoka golini na kuifanya AC Milan iongoze kwa goli 1-0 dakika tano tangu kuanza kwa mchezo.  

Giacomo Bonaventura akaipatia AC Milan goli la pili akiunganisha krosi ya Riccardo Montolivo wakati goli la tatu la AC Milan likifungwa kwa kichwa na beki wa kimataifa wa Colombia Cristian Zapata kuwapa 'The Rossoneri' uongozi wa goli 3-0 kabla ya mapumziko.



Comments