Wachezaji wa Azm Farid Mussa (katikati) na Mudathir Yahya (kulia) wakishangilia goli la pili la Azam kwa staili ya kusujudu
Timu ya Azam FC imevunja mwiko kwa kuifunga klabu ya Tanzania Prisons kwa goli 2-1 kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu uliopigwa leo kwenye uwanja wa Azam Complex, Chamazi jiji Dar es Salaam.
Azam ndio walikuwa wakwanza kuandika bao la kwanza kupitia kwa Kipre Tchetche aliyefunga goli hilo dakika ya 36 kipindi cha kwanza ambalo lilidumu mpaka kipindi hicho kinamalizika.
Kipindi cha pili Prisons walikianza kwa kasi wakitafuta bao la kusawazisha, jitihanda zao zilifanikiwa kwani Jeremia Juma aliisawazishia timu yake na kuufanya mchezo huo kuwa sare ya goli 1-1.
Wakati Tanzania Prisons wakiamini wamefanikiwa kulazimisha sare hiyo ya goli 1-1, Farid Mussa aliifungia Azam bao la ushindi na kuifanya timu yake iibuke na ushindi wa goli 2-1 kwenye mchezo wa kwanza wa ligi kuu ya Vodacom msimu huu.
Azam wanavunja mwiko kwa kuifunga Prisons 'wajelajela' wa Mbeya kwani katika kipindi cha misimu miwili iliyopita timu hizo zimekuwa zikitoka sare hatimaye leo wameweza
kuibuka na ushindi.
Comments
Post a Comment