ARSENE WENGER AMPOTEZEA MOURINHO


ARSENE WENGER AMPOTEZEA MOURINHO

wenger

Hatimaye kocha Arsene Wenger wa Arsenal ameamua kuacha kumjibu kocha mwenye maneno mengi Jose Mourinho na badala yake kuitengeneza Arsenal ishinde michezo yake.

Jose Mourinho aliongea kabla ya michezo ya weekend hii akimponda Wenger kuwa hana presha waliyonayo makocha wengine kwani yuko salama hata kama timu yake ikiwa haishindi makombe, lakini Wenger alikaa kimya na kuipatia ushindi Arsenal wa magoli 5-2 dhidi ya Leicester.

Chelsea wao walitoka sare ya bao 2-2 na Newcastle na kuifanya Chelsea ibakie katika nafasi ya 15 katika msimamo wa ligi huku wenzao Arsenal wakibakiza points 3 tu nyuma ya vinara Manchester United, Arsenal wakiwa nafasi ya tatu.

Alipoulizwa kuhusu maneno ya Mourinho, Wenger alijibu, "hapana, sitaki kujua matokeo ya timu nyingine wala wanachosema makocha wengine. Nina miaka 35 ya ukocha, muhimu kwangu ni kuisaidia timu yangu ishinde".

Mourinho na Wenger wamekua katika vita ya maneno kwa muda sasa, lakini Arsene Wenger ameamua kukaa kimya na kuisaidia timu yake kufanya vizuri.



Comments