ARSENAL WENGER KAMPA TALAKA MKE WAKE…NA PIA WENGER ALIWAI KUWA NA MCHEPUKO HUU


ARSENAL WENGER KAMPA TALAKA MKE WAKE…NA PIA WENGER ALIWAI KUWA NA MCHEPUKO HUU

wenger

Watu maarufu kwenye michezo pia wana maisha yao binafsi na wengine huwa hawapendi sana yazungumziwe kwenye media. Lakini kuna gazeti moja la The Sun, kazi yake kubwa ni kutafuta udaku kuhusu michezo na sio matokeo ya mechi peke yake.

Habari kubwa kwa sasa ni kwamba Arsene Wenger anategemea kumpa talaka mke wake Annie Wenger ambae walifunga ndoa mwaka 2010 na kufanikiwa kupata mtoto wa kike.

Lakini taarifa hiyo inasema kwamba Wenger bado atakua anampa support ya kipesa mwanamke huyu na wameshakubaliana kugawana mali zao.

Licha ya kuwa na mtoto wa kike mwenye miaka 18 lakini inasemakana kwamba wapenzi hao(Arsene na Annie) hawakua na furaha kwenye maisha yao ya mapenzi.

Pia inasemekana kwamba wiki chache kabla ya ndoa yao Arsene Wenger alikua na uhusiano wa siri na msanii mmoja wa kike huko Ufaransa anaitwa Sonia Tatar. Kuachana kwao kumethibitishwa na mahakama za Ufaransa na sasa hivi kila mtu anaweza kuwa na uhusiano na mtu mwingine licha ya Wenger kuendelea kuwa na majukumu ya kulea familia yake hasa mtoto wake.

2CA9E99C00000578-3245488-image-m-47_1442974258840

Sonia Tatar.



Comments