ARSENAL KICHWA CHA MWENDAWAZIMU LIGI YA MABINGWA, YAPIGWA 3-2 NA OLYMPIACOS ...Bayern Munich yaifumua Dinamo Zagreb 5-0
Arsenal wamenyamazishwa kwenye uwanja wao wa Emirates katika mchezo wa Champions League baada ya kufungwa 3-2 na Olympiacos ya Ugiriki.
Matokeo haya yanaifanya Arsenal iburuze mkia katika kundi F baada ya kupoteza michezo yake yote miwili huku Bayern Munich iliyoifumua Dinamo Zagreb 5-0 ikiendelea kujikita kileleni mwa kundi hilo.
Goli la kwanza la Olympiacos lilifungwa na Felipe Pardo dakika ya 33, lakini Theo Walcott akasawazisha dakika mbili baadae kabla ya kipa wa Arsenal David Ospina hajajifunga dakika ya 44.
Alexis Sanchez akaipa uhai Arsenal baada ya kuisawazishia dakika ya 65 na kuwapa mashabiki wao furaha iliyodumu kwa dakika moja kabla ya Alfred Finnbogason hajawafungia wageni bao la ushindi dakika ua 66.
ARSENAL (4-2-3-1): Ospina 4, Bellerin 6.5 (Campbell 86, 6), Gabriel, 6.5, Koscielny 6 (Mertesacker 57, 6), Gibbs 6, Coquelin 6 (Ramsey 60, 6), Cazorla, 6.5, Oxlade-Chamberlain 7, Ozil 6.5, Sanchez 8, Walcott 8
OLYMPIACOS (4-1-4-1): Roberto 7.5; Elabdellaoui 7.5, Botia 8, Siovas 8, Leandro Salino 7; Cambiasso 8.5; Pardo 8, Kasami 8, Fortounis 7.5 (Vouras 87), Seba 7.5 (Hernani 73); Ideye 6.5 (Finnbogason 46, 7)
Muda mfupi baada Alexis Sanchez kufanya mchezo uwe 2-2, Olympiacos wakapata bao la ushindi kupitia kwa Finnbogason
Beki wa Arsenal Gabriel akilala chini kwa huzuni baada mpira kumalizika Emirates kwa kipigo kutoka kwa Olympiacos
Huzuni tupu kwa Gabriel na jezi imekuwa nzito sasa
Winga wa Arsenal Alex Oxlade-Chamberlain akiwa hoi baada ya mchezo
Wachezaji wa Arsenal wakiwa hawaamini kama kweli wachukua kichapo Emirates
Comments
Post a Comment