Anthony Martial kinda wa miaka 19 mwenye thamani ya pauni milioni 58, amezidi kudhihirisha kuwa Manchester United walikuwa sahihi kumsajili kwa bei mbaya baada ya kung'ara kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Southampton.
Katika mchezo huo Martial akaifungia United mabao mawili yaliyochangia ushindi wa 3-2.
Martial alianza kufanya vitu vyake katika mchezo wake wa kwanza kwa Manchester United pale alipotokea benchi na kufunga bao maridadi dhidi ya Liverpool.
Kwa mtaji huo, mshambuliaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa amefunga magoli matatu katika mechi mbili za Premier League, idadi ya magoli ambayo ni sawa na ya Wayne Rooney aliyoifikia ndani ya miezi saba iliyopita.
Southapton ndiyo waliokuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Graziano Pelle ndani ya dakika 13 za mwanzo lakini Anthony Martial akaisawazishia United dakika ya 34 kabla hajatupia la pili dakika ya 5o.
Dakika ya 68 Juan Mata akaifungia United bao la tatu baada ya kumalizia mpira wa Memphis Depay uliogonga nguzo ya goli na kurudi uwanjani huku Graziano Pelle akifunga tena kwa upande wa Southamtpon katika dakika ya 86.
Hata hivyo United inabidi wamshukuru mlinda mlango David de Gea ambaye aliokoa michomo mingi ya wazi ambayo ingeweza kuwapa japo sare Southampton.
Southampton (4-2-3-1): Stekelenburg 6; Yoshida 4.5, Fonte 5.5, van Dijk 5.5, Targett 6 (Martina 46 6); Romeu 6 (S Davis 56 6), Wanyama 6; Ward-Prowse 6 (Long 76 6), Tadić 6, Mané 6; Pellè 7.5
Manchester United (4-2-3-1): De Gea 8; Darmian 5.5 (Valencia 46 6), Smalling 6.5, Blind 5, Rojo 6 (McNair 69 6); Carrick 6 (Schweinsteiger 60 6), Schneiderlin 6; Mata 7.5, Rooney 6, Depay 7.5; Martial 8.5
Martial (kulia) akipongezwa na Juan Mata
Morgan Schneiderlin (kushoto) akimpongeza Martial (kulia) baada ya kuingia United bao la kusawazisha katika uwanja wa St Mary' kwenye mchezo dhidi ya Southampton
Comments
Post a Comment