Mlinzi wa kushoto wa Manchester United Luke Shawa aliumia vibaya wakati wa mchezo wa klabu bingwa Ulaya wakati timu yake ikicheza dhidi ya PSV Eindhoven ya Uholanzi.
Shaw alitolewa nje ya uwanja kwa machela ikiwa ni dakika ya 24 kipindi cha kwanza na nafasi yake kuchukuliwa na Marcos Rojo.
Inaelezwa kuwa Shaw amevunjika mguu na anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mara atakapotua jijini Manchester.
Shaw ameandika kwenye akaunti yake ya Twitter akiwashukuru wale wote walomtumia massages za kumtakia kila la kheri na apone haraka kutokana na jeraha alililopta.
Comments
Post a Comment