Hili ni tegemeo jipya ndani ya Manchester United, kinda Andreas Pereira ameonyesha uwezo wa hali ya juu katika mchezo wa Capital One Cup dhidi ya Ipsiwch.
Kama vile hiyo haitoshi Andreas Pereira akaonyesha uchawi wa Kibrazil kwa kufunga bao tamu la free-kick huku akichanua uwanjani kwa pasi zake zenye macho.
Andreas Pereira ambaye msimu uliopita alizawadiwa tuzo ya mchezaji bora wa U-21, mwenye uwezo wa kucheza kama winga na kiungo mshambuliaji, anatajwa na wachambuzi wa soka kama hazina kubwa ya Manchester United, si kwa miaka ijayo bali hata msimu huu.
Andreas Pereira akifunga kwa free-kick Old Trafford
Hivi ndivyo Pereira alivyouchambua ukuta wa Ipswich Town kwa freek-kick bab kubwa
Pereira akishangilia bao lake
Comments
Post a Comment