MCHEZAJI wa Manchester United Luke Shaw aliyevunjika mguu katika pambano dhidi PSV, alitembelewa hospitalini na Hector Moreno aliyemvunja mguu huo.
Shaw, 20, alitembelewa na Kocha wa PSV Philip Cocu mwishoni mwa juma na mchezaji Moreno ambaye aligonga kwa bahati mbaya katika mfupa wa mguu wa kulia katika mtanange uliomalizika kwa Man Utd kufungwa mabao 2-1.
Cocu alikaririwa akisema: "Hector amejisikia vibaya sana kama binadamu na ndio sababu ya kuja kumtembelea.
"Hata hivyo tulimuuliza Shaw kama tunaweza kumwona akaturuhusu na PSV imetoa msaada kwa ajili yake," alisema kocha huyo wa PSV.
Comments
Post a Comment