Alexis Sanchez alirejea kwenye 'fomu' yake Jumamosi baada ya kuisaida Arsenal kuinyuka Newcastle 5-2 huku akisukumiza wavuni mabao matatu (hat-trick) kwenye mchezo safi wa Premier League.
Kwa alichokifanya Sanchez Jumamosi, akaingia kwenye rekodi ya aina yake baada ya kuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat-trick kwenye ligi kuu za Italia (Serie A), Hispania (La Liga) na England (Premier League.
Hat -trick ya kwanza ya Sanchez ilianzia Italia wakati akiichezea Udinese, February 2011 ambapo alifunga mara tatu katika ushindi wa 7-0 dhidi ya Palermo.
Miezi mitano baadae kiwango chake kikaivutia Barcelona ya Hispania na kumsajili kwa pauni milioni 23.
January 2014 Sanchez akaipigia Barcelona hat-trick kwenye dimba la Nou Camp katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Elche.
Alexis Sanchez amekuwa mchezaji wa kwanza kupiga hat-trick Italia, Hispania na England
Sanchez alianza kupiga hat-trick Udinese ya Italia mwaka 2011 dhidi ya Palermo
Sanchez akafunga hat-trick yake ya pili Hispania akiwa na Barcelona January 2014 dhidi ya Elche
Comments
Post a Comment