WAYNE ROONEY AWATOA SHAKA MASHABIKI WA MAN UNITED, ASEMA MAGOLI YATAMIMINIKA KUTOKA KWENYE MIGUU YAKE
Licha ya kushindwa kuzifumania nyavu msimu huu, mshambuliaji temeo wa Manchester United Wayne Rooney amesema magoli yatamiminika kutoka kwake muda si mrefu.
Rooney, mwenye miaka 29, amecheza kama mshambuliaji wa kati kwenye michezo yote ya ufunguzi wa ligi lakini bado hajafumania nyavu katika mchezo wowote ule.
''Nimekua na mchezo mbaya msimu huu na kila mtu analizungumzia hilo. Nimewahi kuwa na tatizo kama hilo kipindi cha nyuma lakini natumai mambo yatabadilika," alisema nahodha huyo wa timu ya taifa ya Uingereza.
''Ndio kwanza msimu umeanza na tumecheza michezo mitatu peke yake. Nilitarajia haya na natumaini mabao yatakuja,sina shaka na hilo''.
Kocha wa Man United Louis van Gaal aliwaacha washambuliaji Robin van Persie na Radamel Falcao huku akisalia na Rooney, Javier Hernandez pamoja na James Wilson kama washambuliaji pekee Old Trafford.
Comments
Post a Comment