WACHEZAJI WA AZAM WALAMBA MKWANJA MREFU BAADA YA KUTWAA NDOO YA KAGAME



WACHEZAJI WA AZAM WALAMBA MKWANJA MREFU BAADA YA KUTWAA NDOO YA KAGAME
Wachezaji wa Azam FC wakiwa wamelibeba kombe la Kagame

Wachezaji wa Azam FC wakiwa wamelibeba kombe la Kagame

Mara baada ya kikosi cha Azam FC 'wanalambalamba' kutwaa ubingwa wa Kagame kwa kuifunga timu ya Gor Mahia kwa goli 2-0 na kutwaa kitita cha dola za kimarekani 30,000, uongozi wa kikosi hicho  umesema zawadi hiyo inakwenda moja kwa moja kwa wachezaji wa timu hiyo.

"Ni utaratibu wa klabu yetu kwamba, kwanza tunatoa bonasi kwa kila mechi kuanzia hatua ya mtoano. Kwahiyo kuanzia hatua ya robo fainali walikuwa wakipata bonasi kila mechi wakishinda lakini bonasi ya mchezon wa fainali ni zawadi yenyewe iliyoko pale huo ni utaratibu wa Azam FC na hilo limefanyika na wachezaji wamechukua ", amesema mtendaji mkuu wa klabu hiyo Saad Kawemba.

"Hiyo ni hela yao wameifanyia kazi wao na technical bench kwasababu ni jambo ambalo wamelitolea jasho kwahiyo klabu inaheshimu hilo na baada ya mashindano yale CEACAFA huwa wanatoa 'cash', pesa hiyo wamekabidhiwa wenyewe na benchi zima la ufundi".

Wachezaji wa Azam wamepewa mapumziko ya wiki moja na baada ya hapo watarejea kambini kuanza mazoezi ya kujiandaa na mechi ya ngao ya jamii dhidi ya Yanga mchezo unaotajiwa kuchezwa Agosti 22 mwaka huu kufungua pazia la ligi kuu Tanzania bara inayoanza mwanzoni mwa mwezi Septemba  mwaka huu.



Comments