VIDEO: JIONEE BALAA LA SAMUEL ETO’O HUKO UTURUKI



VIDEO: JIONEE BALAA LA SAMUEL ETO'O HUKO UTURUKI
Screen-Shot-2015-08-16-at-00.26.33
Wakati anacheza ligi kuu ya England akiwa na timu za Chelsea na Everton, Samuel Eto'o alionekana kuwa mshambuliaji hatari, ingawa makali yake hayakuwa kama zamani.
Pia Eto'o alionesha uwezo mkubwa alipocheza  klabu ya Mallorca,
Mwisho wa yote, kazi kubwa aliyoifanya Barcelona, Cameroon na Inter Milan huiwezi kusahaulika.
Umri ukiwa umeenda (miaka 34), Mcameroon huyo ameenda Uturuki kumalizia soka lake.
Jana usiku, alicheza mechi ya kwanza katika klabu yake ya Antalyaspor na kufunga magoli mawili katika ushindi wa 3-2 dhidi ya Istanbul Basaksehir.
Katika dakika ya 50, Eto'o  aliufanya ubao usomeke 2-1 akifunga goli maridadi mno.
Dakika 14 baadaye, alifunga goli lingine kwa ufundi wa hali ya juu.
Tazama video ya magoli ya Eto'o



Comments