Katika kile wasichokitegema wananchi wa Madrid walimpita super star wa soka Cristiano Ronaldo ambae alijibadilisha sura na kuwa kama babu omba omba.
Ronaldo alifanyiwa make up kuifanya ngozi yake kuwa kama ya mzee. Pia alivalishwa nywere ambazo zimechoka pamoja na mandevu mengi na mustach. Zaidi ya hapo akavaa manguo mengi yaliyochoka na kuwenda mitaa jiji Madrid.
Kitu cha ajabu ni kwamba omba omba huyu alikua anasakata kabumbu kupita kiasi pale mtaani ambapo watu wakaanza kumshangaa. Wengine walipasiwa mpira lakini walimpotezea.
Dogo mmoja ambae alikua anacheza mpira na ombaomba huyo alipata bahati ya kusaini mpira huo na Ronaldo alivua mandevu na watu wakaanza kumshangaa na kumjalia.
Cheki hii video jinsi ilivyokua.
Comments
Post a Comment