UNAJUA SIRI YA MKALI HUYO BONGO MOVIE KUWA ‘KIBOGOYO’? …Ni Mzee Majanga anayevunja mbavu watu kwa mapengo yake


UNAJUA SIRI YA MKALI HUYO BONGO MOVIE KUWA 'KIBOGOYO'? …Ni Mzee Majanga anayevunja mbavu watu kwa mapengo yake

MCHEZA filamu aliyetokea kuwa gumzo hivi sasa, Filbert Rwambano 'Majanga' ameeleza kuwa, mapengo yake mdomoni ambayo ni kati ya vivutio anapoigiza, yalianza kumchomoka moja moja tangu mwaka 1973 alipokuwa na miaka 21.
Majanga aliyecheza video kadhaa za Juma Nature na PNC, kabla ya kuibuka kwenye muvi ya 'Majanga' alisema kuwa, hivi sasa amesaliwa na meno yasiyozidi kumi mdomoni kwake, huku jingine moja la juu likiwa limeanza kulegea.
Alisema kuwa, kwa kawaida meno yake huwa hayamuumi kama ilivyo kwa wengine wengi, bali huanza kulegea na baada ya siku chache hung'oka hata anapokuwa matembezini.
"Hata hivyo, pamoja na ustaa nilionao, sifikirii kutafuta namna ya kuficha mapengo yangu kwa meno ya bandia, kwasababu sikuzaliwa na meno hivyo sioni aibu," alisema Majanga
Filbert Rwambano 'Majanga' 





Comments