Mario            Balotelli hana nafasi katika kikosi cha Liverpool            kinachofundishwa na Brendan Rodgers na katika ziara ya            maandalizi ya msimu mpya, Muitalia huyo aliachwa akifanya            mazoezi binafsi.
        Jana            wakati Manchester City ikiifumua 3-0 Chelsea katika uwanja wa            Etihad, Balotelli alikuwa miongoni mwa watazamaji.
        Sio            kama mtazamaji wa kawaida,  klabu yake hiyo ya zamani            ilimkaribisha kupitia mtandao rasmi wa Twitter.
        'Nice              of @FinallyMario to pop by today, too!' -Iliandika akaunti              ya Twitter ya Man City.
        Baada            ya ushindi, Straika huyo mwenye utata alionekana akimpongeza            nahodha wa City, Vicent Company ambaye alifunga goli moja kati            ya matatu waliyoshinda.
        Wengine            waliocheka na nyavu ni Sergio Aguero na Fernandinho.
        Kupitia            mtandao wake wa Instagram, Balotelli aliandika"Ni vizuri            kushangilia ushindi na rafiki yako wa zamani"
        'Nice              to celebrate with an old friend.'
        Balotelli aliifungia City magoli          20 ndani ya miaka miwili na nusu aliyodumu Etihad na akauzwa AC          Milan mwezi Januari 2013 kwa dau la paundi milioni 19.
        Wiki ya mwisho kabla ya kufungwa          kwa dirisha la usajili la majira ya kiangazi mwaka jana (2014),          Balotelli alitua Liverpool kwa paundi milioni 16.
        
Comments
Post a Comment