Klabu wanayocheza washambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu TP Mazembe jana ilipata ushindi wake wa kwanza kwenye hatua ya makundi ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani ilipocheza na Smouha ya Misri kwenye mechi yao ya kundi A jijini Lubumbashi.
Roger Assale raia wa Ivory Coast aliibuka shujaa wa mchezo huo baada ya kuifungia timu yake goli muhimu kipindi cha pili cha mchezo huo na kuipeleka Mazembe kileleni mwa Kundi A ikiwa na point inane, pointi tatu zidi ya Moghreb Tetouan ya Morocco na El Hilal ya Sudan. Smouha ambao jana wamepoteza wamepoteza mchezo wao wa watatu mfululizo kwenye hatua ya nane bora wameendelea kusalia mkiani mwa kundi hilo wakiwa na pointi zao tatu.
Ushindi huo umewasogeza Mazembe kwenye ndoto zao za kuhakikisha wanafika hatua ya nne bora na bado wamesaliwa na michezo miwili mkononi.
Smouha waliwaruhusu Mazembe kutawala mchezo huo kwenye umiliki wa mpira huku wenyewe wakishambulia kwa kutumia mipira mipira mirefu pekeyake (counter attack).
Golikipa wa Smouha aliokoa michomo mikali mara mbili wakwati wa kipindi cha kwanza akipangua mpira wa adhabu ndogo uliopigwa na Daniel Nii Adje nje kidogo ya boksi la penati kabla hajafanya kazi ya ziada kuokoa mpira uliopigwa na Adama Traore mchezaji kutoka Mali.
Mazembea waliendelea kulisakama lango la Smouha na mpira uliookolewa na beki wa Smouha Yasser Ibrahim ukatua kwa Mu-ivory Coast ambaye akaiandikia Mazembe goli na kuipa pointi tatu.
Mchezo mwingine wa kundi B uliochezwa Ijumaa, Mohamed Meftah aliihakikisha timu yake ya USM Alger kucheza hatua ya nusu fainali kutokana na oli lake la kichwa kipindi cha pili dhidi ya MC Eulma ambapo USM Alger inafikisha pointi nyingi zaidi ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine na kupata nafasi ya kusonga mbele kwenye michuano hiyo.
Comments
Post a Comment