THIBAUT QOURTOIS AOMBA RADHI MASHABIKI WA CHELSEA


THIBAUT QOURTOIS AOMBA RADHI MASHABIKI WA CHELSEA

RED

Golikipa Thibaut Qourtois wa Chelsea ametumia ukurasa wake wa twitter kuomba radhi kwa wachezaji wenzake pamoja na mashabiki wa chelsea kwa ujumla kwa kupewa kadi nyekundu katika mchezo wao wa ufunguzi wa ligi uliomalizika kwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Swansea katika uwanja wa Stamford Bridge.

Golikipa huyo ameonesha kusikitishwa kwake na kutolewa nje kwa kadi nyekundu hali iliyosababisha Swansea wapate goli la kusawazisha kwa mkwaju wa penati iliyotokana na golikipa huyo kumzuia Bafetimbi Gomis wa Swansea, nafasi ya kufunga bao.

Chelsea walihangaika kutafuta nao la ushindi hata hivyo upungufu wa mchezaji mmoja uliwagharimu na hadi filimbi ya mwisho inapulizwa, matokeo yalikuwa ni mabao 2-2.

Thibaut Qourtois anasema amewaangusha wachezaji wenzake na mashabiki lakini akasisitiza kuwa kwa kuwa ni mara ya kwanza atajitahidi kubadilika na kulinda yasimkute tena yaliyomtokea.

Kuhusu penati hiyo, kipa huyo amekataa kuzungumzia lakini akasema anajutia zaidi kadi nyekundu aliyopewa kwani anaamini angekuwepo uwanjani, lolote lingeweza kutokea.



Comments