Akicheza mechi yake ya            kwanza msimu wa 2015/2016, Lionel Messi hakuhitaji dakika            nyingi kuwanyamazisha mashabiki duniani kote.
        Nyota huyo mwenye miaka            28, raia wa Argentina alifunga magoli mawili kwa mipira miwili            iliyokufa 'Free Kick' Barcelona ikishinda 5-4 dhidi ya Sevilla            katika mechi ya fainali ya Uefa Super Cup iliyopigwa jana.
        Magoli hayo yaliyopishana            kwa dakika 9 tu yaliufanya mtandao wa Twitter uwe 'busy'            kupita maelezo.
        Mshindi huyo mara nne wa            Ballon d'Or, katika maisha yake ya soka hajawahi kufunga free            kick mbili ndani ya mechi moja.
        Kwa kiwango alichoonesha            nyota huyo kijana wa Barcelona, ana uwezekano mkubwa wa            kushinda tuzo binafsi ya tano ya Ballon d'Or mwezi Januari            mwakani.
        Tumekukusanyia baadhi ya            Tweets baada ya Messi kuandika historia ya aina yake.
                

Comments
Post a Comment