TAARIFA RASMI KUTOKA BARCELONA FC…NEYMAR NJE KWA WIKI MBILI


TAARIFA RASMI KUTOKA BARCELONA FC…NEYMAR NJE KWA WIKI MBILI

ney

Hatimaye mtandao wa klabu ya soka ya Fc Barcelona umetanabaisha ya kwamba Mshambuliaji wake hatari kutoka nchini Brazil, Neymar Junior atakaa nje ya dimba kwa muda wa wiki mbili mara baada ya kupata majeraha katika harakati za kujiandaa na mechi ya UEFA super cup dhidi ya Fc Seville.

Hii ina maana mchezaji huyo muhimu atakosa mechi hiyo ya Super cup inayotarajiwa kupigwa tarehe 11 August 2015 kwenye uwanja wa Boris Paichadze Dinamo Arena, katika jiji la Tbilisi , nchini Georgia. Neymar amekuwa akidungwa sindano za Mara kwa mara tangu apate majeraha katika fainali za kombe la dunia.

Neymar ni miongoni mwa wachezaji muhimu wanaotengeneza "partnership" ya MSN huku akiwa sambamba na wenzake Messi pamoja na Suarez. Nafasi yake inatatajiwa kuchukuliwa na Rafinha ama Munir El Haddad.



Comments