SIMBA KUJIPIMA NGUVU TENA LEO ZANZIBAR


SIMBA KUJIPIMA NGUVU TENA LEO ZANZIBAR

simba-sports-club-dylan-kerr1Kikosi cha 'Wekundu wa Msimbazi' Simba leo kitakuwa uwanjani kumenyana na timu ya Jang'ombe Boys ya visiwani Zanzibar kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu ikiwa ni sehemu ya maandalizi kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara inayotarajiwa kuanza mwanzoni mwa mwezi Septemba mwaka huu.

Kiongozi wa kambi ya Simba visiwani humo Abul Mshangama amethibisha kuwepo kwa mtanange huo utakaopigwa majira ya saa 10:00 jioni.

"Leo tunacheza saa 10 ni timu ambayo siku za hivi karibuni imekuwa tishio na gumzo inaitwa Jang'ombe Boys ambao siku si nyingi wameajiri kocha wao kutoka Uturuki", amesema Mshangama.

"Wachezaji wapo vizuri isipokuwa Jonas Mkude bado anamajeraha na anafanya mazoezi mepesi waliobakia wote wapo vizuri", ameongeza.

Simba inatarajia kukamilisha mechi zake za kirafiki visiwani Zanzibar kwa kucheza na KMKM siku ya Jumatano  na kikosi cha Simba kitarudi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maadhimisho ya siku ya Simba Day lakini inadaiwa kuwa, kocha wa kikosi hicho ameomba warejee tena visiwani Zanzibar mara baada ya mapumziko ya wiki moja.



Comments