SHERMAN AIKARIBIA REKODI YA GEORGE WEAH


SHERMAN AIKARIBIA REKODI YA GEORGE WEAH

Sherman Kpah 1

Mshambuliaji mwenye nguvu raia wa Liberia Kpah Sherman amejiunga rasmi na klabu ya Mpumalanga Black Aces kwa mkataba wa miaka mitatu tangu jana asubuhi. Sherman aliisaidia klabu yake ya zamani (Yanga) kutwaa ubingwa wa msimu uliopita kwa kufunga magoli sita kwenye mechi za ligi huku akiwa na assists tano kwenye mechi 16 za ligi ambazo alicheza tangu ajiunge na Yanga katikati ya msimu wakati wa dirisha dogo la usajili.

Sherman yupo hatua moja nyuma ya Mliberia mwenzie George Weah mkongwe wa Afrika ambaye ndiye pekee aliyewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia (balon d'Or) kuoka bara la Afrika. Weah ameweka rekodi ya kutwaa mataji matatu ya ligi kwenye nchi tatu tofauti. Mshindi huyo wa zamani wa tuzo ya mchezaji bora wa dunia alishinda taji la ligi ya Liberia (Liberian Premier League) akiwa na Invincible Eleven na Mighty Barrole kabla ya kushinda taji la ligi ya Italia (Serie A) akiwa na AC Milan na ile ya Ufaransa (French league 1) akiwa na Paris Saint Germain (PSG).

Sherman yeye ametwaa mataji mawili ya ligi kwenye nchi mbili tofauti akianzia Cyprus ambako alishinda taji la ligi kiwa na Centikaya Turk S.K mwaka 2012 kabla ya kufanya hivyo akiwa na Yanga (Tanzania) msimu uliopita.

Aces ilikuwa ikimfutilia Sherman kwa kipindi kirefu na walitaka kumsajili tangu msimu uliopita lakini kwa muda huo ingekuwa ni kinyume na taratibu zao za usajili wa wachezaji wa nje.

Mwenyekiti wa Aces Mario Morfou alivutiwa na mchezaji huyo na alikuwa akiisaka saini yake huku akiamini atakuwa ni moja ya washambuliaji watakaokuwa bora kwenye ligi ya PSL kwa msimu huu.

 "Ni mchezaji mzuri sana na ni kati ya wachezaji bora ambao tumewahi kuwasajili, tunafurahi kumkaribisha rasmi ndani ya AmaZayoni. Atakuwa akishirikiana na Collins Mbesuma kwenye safu ya ushambuliaji ninaimani atakuwa ni miongoni mwa wafungaji bora kwenye ligi msimu huu".

Sherman litambulishwa kwa wachezaji wenzake wa klabu yake mpya ya Aces siku ya Ijumaa na akamaliza siku nzima akiwa na Esau Mtsweni pamoja na Denis Masina na akapata fursa ya kutembelea soko la Aces pamoja na kupata historia ya klabu.

Baada ya yote hayo Sherman akasema: "Ni nchi nzuri nimevutiwa na nilichokiona, nimekuwa nikiona na kusikia kuhusu Black Aces na sasa nimepokelewa vizuri hapa. Niko makini sana kujijenga mwenyewe kwenye timu hii na nataka kukutana na kusalimiana na mashabiki na jamii kama sehemu ya Aces".



Comments