Salim Juma
Fiorentina jana iliibamiza Fc Barcelona magoli 2-1. Kutokana na
matokeo hayo Fc Barcelona mpaka sasa imecheza mechi 4 kwenye mechi za
maandalizi za msimu ila imeambulia ushindi katika mechi moja pekee,
kutokana na ratiba yake ni wazi kuwa Barca wamebakiza mechi moja dhidi
ya As Roma. Kutokana na kiwango chao cha siku zote naamini utaungana
na mimi kuwa hiki sio kiwango cha Barca japokuwa wanakosa wachezaji
wao muhimu kwenye mechi hizi. Leo hii naomba tuangalie kwa ufupi
maeneo matatu ambayo siku zote yamekuwa yakiamua matokeo kwenye mechi
za Barca…
"Fiorentina walicheza vizuri na walikuwa na uwezo. Kuna vitu kwenye
mechi nimegundua, tulikosa umakini golini lakini hatukutengeneza
nafasi nyingi" Maneno ya kocha wa Barca mara baada ya kipigo kingine
pale Artemio Franchi Stadium.
Maeneo yafuatayo yamekuwa yakiamua matokeo katika mechi za Barcelona
siku zote, sio mbaya leo tukiyaangalia kutokana na performance mbovu
ya Barcelona kwenye mechi za pre season.
SAFU YA ULINZI BADO INAMUHITAJI JAVIER MASCHERANO.
Katika mechi 4 ilizocheza Barca imeruhusu magoli 7, tatizo sio kuruhusu tu magoli
haya ila ni jinsi timu inavyocheza pale nyuma. Safu ya ulinzi mpaka
sasa inaonekana imelala, haichezi kwa juhudi na inaruhusu magoli
mengi. Vermalin na Pique mpaka sasa hawachezi vizuri, japokuwa ni
mechi za kirafiki ila aina ya timu walizokutana nazo mpaka sasa ni
timu kubwa ambazo zimezizidi timu kibao za pale Spain, kwa maana hii
ni wazi Enrique anapaswa kupanyia kazi mapema sana kama ana mpango wa
kumtumia Vermalin msimu ujao. Kama hali itakuwa hivi ni wazi itakuwa
…ngumu kutetea makombe yao kwani mpira unabadilika usitegemee kama
msimu uliopita ulimfunga fulani basi na msimu huu utamfunga tena
fulani…! Hilo ni gumu kwa sasa. Japokuwa Alves na Mascherano
hawachezi kwa sasa kutokana na mapumziko waliyopewa ila safu ya ulinzi
inapaswa kucheza kwa juhudi na umakini wa kutosha.
VIUNGO WA FC BARCELONA BADO WANACHEZA KWA JUHUDI KUBWA.
Luis Enrique mpaka sasa ameendelea ku-maintain kiwango cha Barca katika eneo hili
kama Makocha wengine walivyofanya huko nyuma. Inawezekana ni kwasababu
Iniesta, Ractic na Busquet wamecheza mara nyingi kwenye Pre season ila
hata wale walioingia sub akina Munir El Haddadi, Gerald Gumbau bado
wameonekana kucheza vizuri katika eneo hili ambalo siku zote inaleta
Balance ya timu. Kumbuka hata mechi yao dhidi ya Man u walitawala sana
eneo hili vivo hivyo katika mechi ya jana. Inawezekana Partneship ya
Ractic, Iniesta na Busquet ikazidi kufanya vizuri huku Arda Turan nae
akirejea mwezi January bila shaka eneo la kati bado litazidi kusumbua
wapinzani. Mipira mingi ilikuwa inafika kwa wakati eneo la
ushambuliaji pamoja na kwa mawinga. Viungo bado wanafanya maamuzi
sahihi na mashambulizi ya uhakika. Kumbuka Raktic alitoa assist ya
goli jana.
BILA "MSN" HAKUNA KITU PALE MBELE.
Japokuwa Suarez amejitahidi kadiri ya uwezo wake kwa kuwa na magoli 3 mpaka sasa ila pale mbele bado
hapajatulia kwani sio kawaida Barca kufungwa magoli mengi kuliko yale
iliyofunga..! Mfano katika mechi yao ya jana dhidi ya Fiorentina licha
ya kupiga mashuti 22 na kutengeneza nafasi 9 za kufunga, waliambulia
goli moja pekee. Ni wazi eneo hili bado linawasubiri Neymar na Messi
ili kuendeleza mauaji kwani kwa sasa pamefifia kutokana na kutokuwepo
kwa wawili hawa. Katika mechi 4 Suarez kafunga magoli 3, inawezekana
Messi na Neymar kama wangekuwepo basi wangekuwa na idadi sawa ya
magoli kama ya Suarez. Hapa Luis Enrique hatoumiza kichwa sana kama
kwenye safu ya ulinzi.
Kutokana na maeneo hayo matatu ni wazi kuwa eneo la nyuma bado sio
zuri katika mechi hizi za pre season, Waswahili wanasema Nyota njema
huonekana asubuhi, tumewaona Arsenal kwenye mechi kama hizi walikuwa
na safu nzuri ya ulinzi, hilo pia limeendelea kwenye mechi yao dhidi
ya Chelsea…! Fc Barcelona wanapaswa kuwa na safu nzuri pale nyuma
hata kama Mascherano hayupo kule nyuma kwani inawezekana ipo siku
akakosa mechi muhimu na Enrique akapata shida kama aliyopata kwenye
mechi hizi 4 mpaka sasa.
Comments
Post a Comment