Gary Neville ameponda makosa endelevu ya kushindwa kutafsiri sheria mpya ya kuotea katika michuano ya ligi kuu England kufuatia Liverpool kupewa goli lisilostahili kwenye mchezo wa EPL uliopigwa Jana usiku dhidi ya Bournemouth.
Goli pekee la Christian Benteke katika uwanja wa Anfield lilitakiwa kukataliwa kwasababu mchezaji mwenzie, Philippe Coutinho alikuwa tayari ameotea.
Siku chache kabla ya msimu mpya kuanza, yalifanyika mabadiliko ya sheria ya kuotea ambapo mchezaji yoyote anayecheza mpira katika eneo la kuotea, kibendera lazima kiwe juu na hata kama hakugusa mpira.
Mwamuzi msaidizi, Harry Lennard alishindwa kunyosha kibendera, akimuacha Benteke afunge.
Neville amedai makosa haya ni stori za kila msimu na kila msimu mpya wanakuja na mabadiliko lakini hakuna wanachofanya.
Comments
Post a Comment