Arsene Wenger tangu ajiunge na klabu ya Arsenal mnamo mwaka 1996 amewapa nafasi wachezaji kadhaa kukichezea kikosi hicho,Petr Cech alikuwa mchezaji wa 199 kuichezea Arsenal mchezo wa kwanza akiwa chini Wenger,katika kipindi hicho chote
kama mshambuliaji kinda Alex Iwobi angepewa nafasi ya kucheza hapo jana kwenye mchezo dhidi ya Chelsea basi angekuwa mchezaji wa 200.
kikosi cha kwanza cha Wenger mara tu baada ya kujiunga Arsenal kilikuwa na nyota kama vile David Seaman, Tony Adams, Ian Wright na Martin Keown,kikosi hicho kilishinda mabao 2-0 dhidi ya Blackburn.
Mchezaji mgeni wa kwanza kuicghezea Arsenal chini ya Wenger alikuwa Patrick Vieira, Mfaransa wa kwanza kati ya 26 walioichezea Arsenal katika kipindi cha utawala wa Wenger.
Wachezaji wafuatao namba zao kwenye mabano ni miongoni mwa wanandinga walioichezea timu iyo kwenye utawala wa Wenger,Dennis Bergkamp (13th), Thierry Henry ( 48th),Alexis Sanchez (193), Mesut Ozil (183),Santi Cazorla (173),
Tomas Danilevicius (65),Patrick Cregg (106).
Comments
Post a Comment