MUSONYE, MGOI, ALMANUSURA KUZICHAPA ‘KAVUKAVU’ KISA….



MUSONYE, MGOI, ALMANUSURA KUZICHAPA 'KAVUKAVU' KISA….
Katibu wa CECAFA NIcolus Musonye akizungumza na              waandishi wa habari

Katibu wa CECAFA Nicolus Musonye akizungumza na waandishi wa habari

Katibu mkuu wa CECAFA Nicolus Musonye na mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Kagame Ahmed Msafirri Mgoi jana almanusura wazichape 'kavukavu' uwanja wa taifa pale walipohitilafiana kwa mambo kadhaa kuhusiana na mashindano hayo yaliyofikia tamati jana kwa Azam kuwa mabingwa wapya wa mashindano hayo.

Mgoi alidai kwamba, Musonye alikuwa anashinikiza Raira Odinga ndie awe mgeni rasmi kwenye fainali hiyo wakati TFF wao walisha mwandaa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Meck Sadick ndie awe mgeni wa heshima wa fainali hiyo jambo lililopingwa vikali na Musonye.

Ikumbukwe kuwa, Odinga alipata nafasi ya kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano hayo baada ya aliyealikwa kuwa mgeni rasmi Waziri wa Ujenzi Dkt. John Magufuli kushindwa kuhudhuria kwenye ufunguzi wa michuano hiyo.

Katika hatua nyingine Mgoi amesema timu ya Gor Mahia iligoma kutumia vyumba vya kubadilishia nguo na kukaa sehemu ambayo hairuhusiwi kwa madai kwamba kwenye vyumba walivyokuwa wameandaliwa kulikuwa kumepulizwa dawa kwa ajili ya kuwadhuru wachezaji wa timu hiyo. Inadaiwa kuwa kocha msaidizi wa Gor Mahia aliharibu kitasa cha mlango ili kuhakikisha kuwa haufunguki ili wasiingie kwenye vvyumba hivyo.

Musonye pia anadaiwa kuwa alikuwa anapambana kutengeneza mazingira ya kuhakikisha Gor Mahia inapata ushindi kwenye mchezo wa fainali hali iliyozua sintofahamu kati yao na kufikia kukunjana mashati kwa viongozi hao.

Hizi hapa sauti za Mgoi na Musonye kila mmoja akieleza nini tatizo hadi kufikia hatua kutaka kuzichapa…




Comments