Jose Mourinho alirusha medali yake ya Community Shield kwa mashabiki na kusema kwamba medali hiyo ni ya losers kwa hiyo haitaki. So hakutaka kuondoka nayo na kuwarusha kwa mashabiki waigombanie.
Sasa aliyeidaka ni dogo ambae alikuwa uwanjani kushabikia club ya Arsenal na timu yake ikashinda. Hii sio mara ya kwanza kwa Jose kufanya hivi kwasababu aliwai kufanya hiki kitendo waliposhinda ubingwa wa EPL kabla hajaiacha Chelsea kuelekeaa Real Madrid. Sababu aliyoitoa sasa hivi ni kwamba medali ile ni kwa ajili ya losers na kipindi kile alisema anataka kushinda UEFA na sio ligi tena.
Comments
Post a Comment