MASIKINI MOURINHO….! NDOTO ZAKE KUFANYA KAZI NA DZEKO ZAOTA MBAWA



MASIKINI MOURINHO….! NDOTO ZAKE KUFANYA KAZI NA DZEKO ZAOTA MBAWA

Dzeko Edin

 Na Salym Juma

Baada ya kuchoka na mihangaiko ya kila siku niliamua kuchukua Kompyuta pakato (laptop) na kuangalia video za soka ambazo zinatazamwa sana mitandaoni. Mara nyingi napenda kuangalia zile ambao hazizungumzwi lakini ni kali..! Nilijikuta naangalia video moja kati ya Belgium na Bosnia..!
Hapa Mtangazaji anatangaza goli 1 hadi analia kwa furaha…! Goli hili ni la Mzungu mmoja aliyevaa jezi namba 11 anawalamba vyenga Mabeki kibao anafanya kama anapiga, kumbe anapita.., anapiga mashuti makali sana, nawaona mabeki wa Belgium wanachanganyikiwa mwisho anatupia goli kwenye nyavu kule juu kabisa wanapotagia Ndege……

Kutokana na kiwango cha huyu jamaa nalazimika kumsikiliza 'Comententor' kwa makini ili kufahamu jina la huyu Mzungu mrefu mwembamba ambaye nasikia imani yake ya dini ni ile ya akina Franky
Ribery na Adnan Januzaji..! Japokuwa 'Comentetor' anatangaza hili goli kwa hisia ila mwisho nasikia jina lake…!! duuu.! kumbe ni huyu……

Aliwahi kuwa Mchezaji wa kwanza kuifungia Man City magoli manne katika mechi moja kwenye EPL. Kwa mwaka 2011 usajili wake kuja EPL ndio usajili wa pili kwa ukubwa baada ya ule wa Robinho, pia ulikuwa usajili mkubwa kwa pale Bundesliga. Kipindi cha nyuma alikuwa anacheza nafasi ya kiungo..! Kuna katuni ya gazeti moja la Italia ilimuonesha akimpigia simu Tevez kuwa anakwenda Italia muda mchache baadae Tevez akaanza kutafuta dili la kurudi kwao…..

Hapa namzungumzia raia wa Bosnia aliyekuwa anawindwa na Jose Mourinho kwa muda mrefu, naomba tuwe wote hadi mwisho wa makala hii kuzungumzia 'point' hii ya Mourinho na Dzeko, nukta ambayo 'media'nyingi za Ulaya zimekaa kimya hadi leo licha ya kufahamu ni kwa jinsi gani Mou anamkubali Dzeko..

"Mchezaji wangu bora wa mwaka siku zote anatokea kwenye timu iliyochukua ubingwa. Ninasema mchezaji wa Man City Dzeko. Alikuwa ni mshambuliaji chaguo la tatu mwanzoni mwa msimu wakati timu inamuhitaji
na alionesha tofauti. Alikuwa na magoli 16. Kumi na sita kwa mshambuliaji chaguo la tatu ni jambo la kuvutia. Sio mfungaji pekee pia anatoa assists na anacheza vizuri".

"Ana tabia nzuri, yupo fair, hajirushi ovyo uwanjani, hapendi kuwatafutia wapinzani kadi" Alimaliza Mourinho maneno haya siku ya Jumapili tarehe 10/5/2014.

Akiwa Wolfsburg Eden alikuwa ni miongoni mwa washambuliaji kuntu kwani katika mechi 32 za msimu wake wa pili alitupia magoli 26 na kutoa assists 10. Kutokana na kiwango hiki, timu yake ilichukua ubingwa wa
ligi kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa kwa timu hiyo. Pia kama kumbukumbu zako ziko vizuri utakumbuka kipindi hiki alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa Bundesliga hii ilikuwa baada ya kutupia magoli sita katika mechi mbili za DFB-Pokal, magoli manne na assist mbili katika mechi nane za UEFA.

Pia hapa hapa Ujerumani alikuwa mfungaji bora wa ligi na kukataa ofa ya kujiunga na klabu ya Ac Milan. msimu wake wa mwisho akiwa Ujerumani alitupia magoli 10 katika mechi 17 huku akitengeneza historia kwenye timu yake baada ya kutupia magoli 59 katika mechi 96..! Nani mwingine
amefanya hivi pale Wolfsburg?? Hapa ndio Roberto Mancini alipotokwa udenda na  kutoa pauni milioni 27 kumvuta Etihad huku ukiwa usajili wa juu kufanywa na Man City kwa kipindi hiki cha 2011 baada ya ule wa Robinho kutoka Madrid. Hapa ndipo alipokuja kuanza safari yake kwa shida sana EPL hadi alipoondoka sambamba na mwenzake Jovetic.

Edez Dzeko alikutana na washambuliaji hatari duniani "World class
strikers" pale Etihad, kumbuka kipindi hiki walikuwepo Baloteli (Super Mario),Tevez na Aguero..! Kwa viwango vya watu hawa unadhani Eden angepata nafasi kama ile aliyokuwa anaipata Wolsfburg? Hapa ndio mahali kiwango chake cha kutupia nyavu kikaanza kushuka. Japokuwa alikuwa na wakati mgumu kumbuka alikuwa mfungaji bora wa Man City msimu wa 2012-13 akiwa na magoli 15 katika mechi 44. Hata baada ya kuondoka Tevez na Baloteli bado washambuliaji wenye viwango kama Jovetic na Wilfred Bony walikuja kuzidi kuhatarisha maisha yake pale Etihad.

Japokuwa mwaka jana alisaini mkataba mpya ni wazi kuwa Dzeko amechoshwa na kusubiri mpaka Aguero, Jovetic na Bony wasiwe vizuri ndipo apate uhakika wa kucheza muda wote, kutokana na usajili wa
Raheem ambaye inasadikika ataenda kuwa 'partner' wa Aguero ni jambo la kheri Pellagrin kumruhusu aende akatafute maisha mapya kwenye ligi ya Italia baada ya As Roma kumsajili kwa pauini milioni 14, japokuwa alikuja kwa pauni milioni 27 sio mbaya kuondoka kwani kafanya kazi nzuri kwa kutupia magoli 72 katika mechi 187, kumbuka mechi nyingi alikuwa anatokea kama 'sub' hapo ndo utajua uwezo wa huyu jamaa ambaye anatoka Bosnia…!

Tuachane na hayo ya Dzeko, sasa naomba tumuangalie Jose Mourinho..! Tangu kurudi darajani bado hajapata 'striker'  wa uhakika hasa kutokana na Diego kuwa na 'Pancha' za mara kwa mara. Louic Remy bado ni wale
wale kama Diego.! Nilishangaa sana Mou kumuacha Dzeko aende zake na kumchukua kwa mkopo Falcao. Japokuwa umri wa miaka 29 ni ngumu Chelsea kukupa mkataba mnono ila ili kuweza kupata magoli 20 ya uhakika kwa msimu ni wazi Jose alipaswa kumshawishi kipenzi chake Dzeko kwenda darajani na kuwa chaguo la pili baada ya Costa.

Japokuwa Aguero ni mshambuliaji hatari ila hadi kesho Mou anaamini Dzeko ni bora kama akipata nafasi muda wote. Kumbuka Chelsea mchezaji akiwa na miaka 30 hupewa mkataba wa mwaka mmoja, Dzeko ana miaka 29, hapa ndio palileta utata..! Pia kuna taarifa za chini chini kuwa City walikataa kumuuza Dzeko darajani kwa kuwa Chelsea ni wapinzani wao kwenye mbio za ubingwa licha ya Mou kumtaka Dzeko kimya kimya bila kuweka wazi hadharani, kumbuka kuna kipindi usajili wa Falcao kuja Chelsea ulitulia hadi watu wakasahau, kipindi hiki Mou ndo alikuwa ana 'fight' kumchukua Dzeko bila mafanikio..!

Japokuwa Dzeko kaondoka na kushindwa kunaswa na Jose, ni busara aende kuwafundisha adabu mabeki wa Serie A na hatimaye kumaliza msimu akiwa na magoli zaidi ya 20, kuna uwezekano Dzeko akaenda kufanya makubwakwani pale Roma atakuwa na uhakika wa kucheza kwa uhuru japokuwa mshahara wake utakuwa mdogo tofauti na ule wa pale Etihad. Kila lakheri 'brother' Dzeko Mungu akutangulie sisi mashabiki tunasubiri
makubwa kutoka kwao maana kipaji chako hakielezeki.



Comments