Afisa habari wa klabu ya Simba Hajji Manara jana alikuwa kivutio kikubwa kwenye siku ya Simba Day pale alipoingia uwanja kuonesha kipaji chake cha soka wakati timu yake ya viongozi wa Simba SC ilipokuwa ikicheza na wacheza filamu wa Tanzania (Bongo Movies) mchezo uliokuwa wa utangulizi kabla ya mechi ya Simba SC haijacheza na Sports Club Villa ya Uganda.
Manara aliingia uwanjani akitokea benchi na mara baada ya kuanza kucheza mpira mashabiki wa timu hiyo walianza kumshangilia Manara ambaye amekuwa na maneno mengi tangu alipopewa wadhifa wa kuwa afisa habari wa klabu hiyo.
Hata hivyo Manara hakucheza dakika zote zilizokuwa zimesalia kwani alitoka na nafasi yake kuchukuliwa na kiongozi mwingine wa klabu hiyo.
Manara alisema mbali na kuwa msemaji wa Simba, yeye anakipaji cha kucheza mpira na amekuwa akicheza mpira tangu shule ya msingi.
Viongozi wa klabu ya Simba walifanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0 mbele ya waigizaji wa Bongo movies goli lililowekwa kambani na kocha mkuu wa Simba SC Dylan Kerr.
Comments
Post a Comment